Cirque du Soleil kuonesha maigizo ya maisha ya Lionel Messi

|
Lionel Messi ndiye kinara wa mabao wa wakati wote kwa klabu ya Barcelona.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina na nyota wa mabingwa wa Hispania, Barcelona Lionel Messi anatarajia kuigizwa kwenye onyesho la vikaragosi la Cirque du Soleil.

Kundi hilo linatarajia kuwa na onyesho la kimataifa mwakani na limeahidi kufanya “tafsiri ya kisanii ya maisha na kipaji cha hali ya juu cha Lionel Messi”

Cirque du Soleil lenye makazi yake nchini Marekani kwenye mji wa Montreal limewahi kuwaigiza mastaa wengine wengi wakiwemo wa kundi la muziki wa rock la Uingereza la The Beatles na mfalme wa Pop duniani, Michel Jackson.

Lionel Messi akizungumzia onesho hilo amesema "Inachanganya, ni kama jambo la pekee sana lakini ni kama wendawazimu kuona Cirque du Soleil watatengeneza onesho kwa kuangazia maisha yangu, ninachokipenda na mchezo wangu,”.

Messi mwenye tuzo tano za dunia za Ballon d'Or ameelezea maonesho ya kundi hilo kama “kipindi pendwa” nyumbani kwake.

"Sina mashaka onesho hilo litawaacha watu midomo wazi kama ambavyo maonesho yao mara zote hufanya hivyo." Aliongeza Messi

Soka
Maoni