Eden Hazard akiri kuchanganyikiwa juu ya kubaki Chelsea au kujiunga Madrid

|
Eden Hazard amekuwa na msimu mzuri chini ya kocha mpya Maurizio Sarri akiwa na magoli manane katika mechi 10 alizocheza hadi sasa.

Kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji Eden Hazard amesema ‘anachanwa chanwa’ na uamuzi anaopaswa kuchukua kati ya kuongeza mkataba na klabu yake ya sasa ya Chelsea au kujiunga na Real Madrid.

Hazard anatarajiwa kuingia kwenye mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Chelsea mwishoni mwa msimu huu lakini ameendelea kusisitiza asingependa kupita njia aliyoichagua aliyekuwa shujaa wa miamba hiyo ya London, golikipa Thibaus Courtois aliyelazimisha auzwe kwa miamba ya Hispania Real Madrid.

Kiungo huyo aliyeisaidia Ubelgiji kushika nafasi ya tatu kwenye Kombe la Dunia, amesisitiza kuwa yuko tayari kujadiliana juu ya mkataba mpya na Chelsea.

Tetesi za staa huyo aliyeanza msimu huu vizuri akiwa na magoli manane katika mechi 10 alizoheza msimu huu za kuhamia Hispania zilianza kusambaa mwishoni mwa msimu uliopita na wakati wa Kombe la Dunia alithibitisha kutamani kujiunga na Real Madrid.

"Ndio maana nilisema baada ya Kombe la Dunia na nilisema, nafikiri ni wakati wa kubadilisha mazingira kwasababu nilikuwa na wakati mzuri kwenye Kombe la Dunia” alisema Hazard

"Niko vizuri sana kimchezo kwa sasa, ninacheza soka maridadi sana. Real Madrid ni klabu bora zaidi duniani. Sitaki kudanganya hii leo.

"Ni ndoto yangu tangu nikiwa mtoto. Nilikuwa naiota klabu hii. Sitaki kuzungumzia hilo kila siku. Tutaona kitakachotokea” Aliongezea

Hazard ameshinda mataji mawili ya Ligi Kuu Uingereza ‘Premier League’ akiwa na Chelsea, kombe la FA, kombe la Ligi na kombe la Europa.

Soka
Maoni