JPM akutana na timu ya wataalamu kutoka Morocco

|
Rais John Magufuli akijadiliana na watalaamu kutoka Morocco waliofika kwa ajili ya mazungumzo ya kuanza kwa ujenzi wa uwanja wa michezo Dodoma

Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Timu ya wataalamu wa Tanzania na Morocco wanaoshughulikia ujenzi wa uwanja wa michezo katika Jiji la Dodoma, unaotarajiwa kujengwa kwa msaada wa Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI.

Timu hiyo imekutana na Rais Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam, ukiwa umeongozana na Balozi wa Morocco nchini, Abdelilah Benryane.

Mara baada ya kukutana na Rais Magufuli kiongozi huyo amesema pamoja na kuzungumzia uhusiano mzuri wa Tanzania na Morocco wamejadiliana kuhusu utekelezaji wa miradi iliyokubaliwa wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco nchini mwaka 2016 ikiwemo ujenzi wa Msikiti wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa Jijini Dar es Salaam na kuanza kwa ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu Jijini Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale amesema uwanja huo utajengwa jirani na eneo la Nanenane kando ya Barabara ya Dodoma – Morogoro na utajengwa kwa mfano wa mlima Kilimanjaro na utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji kati ya 85,000 na 100,005.

Utawala
Maoni