Kivumbi cha La Liga kutimka kuanzia leo

|
Mtanange wa leo live kupitia Azam Sports HD

Kivumbi cha Ligi kuu soka nchini, Hispania, La Liga kinaendelea kushika kasi leo saa 5:00 usiku kwa mechi moja kupigwa na utaishuhudia mbashara kupitia Azam Sports HD na Azam TV App.

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya 19, inazikutanisha Getafe dhidi ya Malaga, mchezo utaopigwa katika dimba la Coliseum Alfonso Perez katika jiji la Getafe, Madrid.

Malaga ambayo iko nafasi ya 19 ikiwa na pointi 11, inahitaji kutumia mchezo huo kujiondoa kwenye nafasi mbaya iliyopo sasa, wakati Getafe inatafuta mwanya wa kupambana na vigogo walio katika nafasi za juu, kwani hadi sasa katika michezo 18 iliyocheza, imejikusanyia pointi 23 na iko nafasi ya 11.

Timu hizi zinakutana leo huku kila moja ikiwa na machungu ya kupoteza mchezo wake uliopita ambapo Getafe iliyokuwa ugenini ilifungwa 2-0 na Atletico Madrid wakati Malaga ikifungwa nyumbani 1-0 na Espanyol.

Ligi hiyo itaendelea kesho Jumamosi (Januari 13, 2018) kwa mechi nne ambazo ni:-

Girona vs Las Palmas

Real Madrid vs Villarreal

Eibar vs Atletico Madrid

Deportivo La Coruna vs Valencia

Jumapili (Januari 14) pia kutakuwa na mechi nne ambazo ni:-

Levante vs Celta Vigo

Alaves vs Sevilla

Espanyol vs Athletic Bilbao

Real Sociedad vs Barcelona

Raundi hiyo itahitimishwa Jumatatu kwa mchezo mmoja kati ya Real Betis dhidi ya Leganes.

La Liga
Maoni