Kufuzu Olimpiki: Twiga Stars yavutwa shati na DRC

|
Lilipofungwa bao la pili la Twaiga Stars katika sare ya mabao 2-2 dhidi ya DRC, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Timu ya soka ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, imeanza kwa sare ya mabao 2-2 kampeni ya kusaka tiketi ya Kufuzu Olimpiki ya Tokyo 2020 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Magoli ya Tanzania yamefungwa na Donesia Daniel dakika ya 46 na Asha Rashid dakika ya 79, huku mabao ya DRC yakiwekwa kimiani na Marilene Yav dakika ya 11 na Grace Balongo dakika ya 54.

Kwa matokeo ya leo, Twiga Stars, itahitaji ushindi wa bao 1-0 ugenini ili iweze kuitupa nje DRC, hivyo, benchi la Ufundi na Watanzania wanatakiwa kuwapa sapoti zaidi akina dada hao ili waende Olimpiki ya Tokyo 2020.

Soka la wanawake
Maoni