Lipuli yaichapa African Lyon 5-0 mechi ya kulinda tembo

|
Takwimu za mchezo

Mechi maalum ya kirafiki ya kupinga ujangili na mauaji ya tembo kati ya Lipuli FC na African Lyon imechezwa leo kwenye Uwanja wa Samora Mjini Iringa ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga.

Katika mchezo huo ambao ulibeba kampeni ya Linda Tembo, Wanapaluhengo wameibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0.

Issa Rashid amefunga magoli mawili katika dakika ya 13 na 35, huku mabao mengine yakiwekwa kimiani na Daruesh Saliboko dakika ya 14, Keneth Masumbuko dakika ya 26 na Mussa Nampaka Chibwabwa dakika ya 85.

Lipuli FC wamekabidhiwa kombe, huku viongozi wa kiserikali wakizishukuru timu hizo za ligi kuu kukubali kuwa sehemu ya kampeni hii muhimu ya kimataifa ya kulinda Tembo.

Soka
Maoni