Lipuli yasaka heshima kwa Mtibwa Sugar leo

|
Mtibwa Sugar vs Lipuli FC, LIVE Azam Sports 2.

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo, Jumatano kwa mchezo mmoja, ambapo Mtibwa Sugar FC wataikaribisha Lipuli FC kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro. 

Mchezo huo ni wa raundi ya 28, na utakuwa mbashara kupitia Azam Sports 2.

Kikosi cha Lipuli FC kinatarajiwa kuongozwa na straika wake, Adam Salamba ambaye amekuwa akiombwa na klabu ya Yanga ili kuisaidia kwenye mechi za kimataifa.

Mchezo huo ni wa kusaka heshima kwani kila timu ipo salama na ina uhakika wa kucheza tena ligi kuu msimu ujao, Lipuli wakiwa na pointi 32 katika nafasi ya nane huku Mtibwa wakiwa na pointi 37 katika nafasi ya sita.

VPL
Maoni