Liverpool kujaribu bahati yake kwa Wolves Emirates FA Cup

|
Timu hizi zilipokutana kwenye hatua kama hii mwaka 2011, Liverpool alipigwa mabao 2-1.

Raundi ya tatu ya michuano ya Kombe la FA (Emirates FA Cup) inaendelea leo kwa Liverpool kucheza ugenini dhidi ya Wolves mchezo ukipigwa majira ya saa 4:45 usiku na kukufikia LIVE kupitia Azam Sports 2.

Haya ni mambo sita unayopaswa kuyafahamu kuhusu timu hizi.

  1. Leo itakuwa ni mara ya saba kwa timu hizi kukutana, Wolves ikiwa imeshinda mechi nne kati ya sita zilizopita ikiwemo ile waliyokutana kwenye hatua kama hii mwezi Januari 2017 ambayo Wolves ilishinda 2-1 kwenye Uwanja wa Anfield.
  2. Kwa mara ya mwisho timu hizo zimekutana Desemba 21, 2018 katika mchezo wa EPL na Liverpool kushinda mabao 2-0.
  3. Liverpool imeondolewa kwenye mashindano hayo mara tano kati ya saba ambazo imekutana na timu inazoshirikinazo ligi kuu.
  4. Wolves hawajashinda mchezo wowote kati mechi sita za Kombe la FA ilizocheza nyumbani ikiwa imepoteza mechi mbili na kutoka sare mechi nne. Mchezo wa mwisho kushinda ni dhidi ya Doncaster katika msimu wa 2010/11.
  5. Liverpool imefika fainali ya michuano hii ya FA mara 14 na kuchukua ndoo mara saba ambapo mara ya mwisho ilikiwa mwaka 2006.
  6. Liverpool haijawahi kuondolewa kwenye mashindano haya katika hatua hii ya raundi tatu tangu msimu wa 2010/11 ilipochapwa 1-0 na Man United.

Je, leo majogoo hawa watafanya nini?

Ni Wolves vs Liverpool saa 4:45 usiku LIVE Azam Sports 2

Emirates FA Cup
Maoni