Maafande wa Magereza wawachapa Maafande wa JKT ligi kuu

|
Kocha Msaidizi wa Tanzania Prisons, Elly Boimanda.

Wajelajela wa Tanzania Prisons wameendeleza ubabe kwenye uwanja wao wa nyumbani Sokoine jijini Mbeya baada ya kuwatembeza kwata maafande wenzao Jeshi la Kujenga taifa (JKT Tanzania) kwa mabao 2-0.

Goli la kwanza limetiwa kimiani na Vedastus Mwihambi mnamo dakika ya 21 kipindi cha kwanza kabla ya Adam Adam kuiandikia timu yake goli la pili mnamo dakika ya 61 kipindi cha pili.

Katika mchezo mwingine uliopigwa leo, Mwadui FC imeshindwa kutamba Mbele ya Stand United baada ya kukubali kichapo cha magoli 2-1 kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.

Bao pekee la Mwadui limewekwa kimyani na Salim Aiyee ambaye anaendelea kuwa kinara wa ufungaji akitupia mabao 16 mpaka sasa huku magoli ya Stand yakifungwa na Datius Peter na Jacob Masawe.

Mechi ya tatu iliyopigwa leo kuanzia majira ya saa 1:00 usiku imewakutanisha Azam Fc waliokuwa wenyeji wa Singida United kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

TPL
Maoni