Wanyama akanusha uvumi wa kuhamia Liverpool

|
Victor Wanyama

Kiungo wa klabu ya Tottenham na timu ya taifa ya Kenya, Victor Wanyama amesema tetesi zilizopo kuwa msimu ujao huenda akaonekana kwenye uzi wa klabu ya Liverpool si za kweli.

Akiongea na moja ya kituo cha runinga jana, Wanyama ambaye yuko nchini kwa mapumziko mafupi amesema tetesi hizo siyo za kweli  na kwamba yeye bado ni mchezaji wa Tottenham na ataendelea kuwepo klabuni hapo.

''Mimi bado ni mchezaji wa Tottenham na nina mkataba na timu hiyo kwa hiyo, nipo pale bado hizo ni tetesi tu ila ukweli mimi nitacheza pale msimu ujao'', amesema. 

Wanyama ambaye ni raia wa Kenya yupo nchini baada ya ligi kuu nchini England kufika tamati kwenye msimu wa 2017/18. Tottenham imemaliza katika nafasi ya tatu (3) ikiwa na alama 77. 

Kiungo huyo anayesifika kwa ukabaji, ameahi kucheza soka katika ligi tofauti ikiwemo Ubelgiji anakocheza Mbwana Samatta pamoja na Scotland kabla ya kutua rasmi nchini England.

Soka
Maoni