Mbabe kati ya Fury na Wilder kujulikana Desemba 2

|
Deontay Wilder (kushoto) alipotaka kuzichapa kavukavu na Tyson Fury wakati wa zoezi la kupima uzito.

Alfajiri ya kuamkia kesho Desemba 2, 2018, Bondia Tyson Fury anapanda Ulingoni kucheza pambano kubwa dhidi ya Bingwa wa Dunia wa Masumbwi ya  uzito wa juu mkanda wa WBC, Deontay Wilder katika Ukumbi wa Los Angeles' Staples Center nchini Marekani.

Mabondia hao wawili jana wamepima uzito ambapo Fury ana Kilogram 116 huku Wilder wa Marekani akiwa na Kilogram 96.4 na almanusuru wazichape kavukavu baada ya kutambiana sana.

Wilder atakuwa anatetea mkanda wake wa WBC kwenye pambambo hilo linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa ngumi za uzito wa juu, huku Fury akidai atatoa kichapo kama alivyofanya kwa Wladimir Klitschko mwaka  2015.

Hata hivyo, Wilder ni Bingwa wa ngumi za uzito wa juu na mshindi wa zamani wa medali kwenye Olimpiki na hajawahi kupigwa katika mapambano 40 aliyocheza, huku akiwa na nguvu za ajabu katika mkono wake wa kulia.

Naye Fury ni mwamba wa sawasawa ambaye ameshinda mapambano yake yote 27 aliyopanda ulingoni, hivyo pambano lao linategemewa kuwa na mvuto mkubwa.

Ngumi
Maoni