Mechi tatu VPL kupigwa leo

|
Mechi hii itakuwa LIVE Azam Sports 2.

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inaendelea leo kwa michezo mitatu itakayopigwa katika viwanja tofauti kukamilisha mzunguko wake 25.

Katika dimba la Taifa Dar es Salaam, Simba SC inawakaribisha Tanzania Prisons mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani wa aina yake kutokana na Simba kuwa kwenye mbio za ubingwa msimu.

Wakati Simba wakitamani kujiongozea pointi tatu muhimu, Tanzania Prisons ambao wapo kwenye kiwango kizuri msimu huu, wamepania kuikwamisha Simba na kuivunjia rekodi yake ya kutopoteza mchezo tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi.

Hadi sasa Simba ndiyo vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 55 kwa mechi 23 walizocheza wakati Tanzania Prisons wako nafasi ya nne wakiwa na pointi 38 kwa mechi 24 walizocheza.

Mechi nyingine zitakazopigwa leo ni pamoja na Kagera Sugar ambao wako nyumbani kuikabili Mtibwa Sugar kwenye dimba la Kaitaba Bukoba, huku Ndanda FC wakiwa nyumbani kuikaribisha Ruvu Shooting.

VPL
Maoni