Mkutano Mkuu TFF: Wajumbe wapya waapishwa

|
Stephen Mguto akiapa kuwa Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF.

Mkutano Mkuu wa TFF umefanya uchaguzi wa kuziba nafasi ya mjumbe wa kamati yake ya utendaji akiwakilisha Kanda ya Shinyanga na Simiyu ambapo Osuri Charles Kosori ameshinda kwa kura 91 akiwapiku Benister Rugora aliyepata kura 20 na Kanjanja Magesa aliyepata kura 17.

Pia mkutano huo umewaapisha wajumbe wapya wa kamati ya utendaji ambao ni Ahmed Msafiri Mgoyi na Athuman Nyamlani ambao wameteuliwa na Rais wa TFF.

Mwingine aliyeapishwa na Stephen Mguto ambaye anakuwa mjumbe wa kamati hiyo kutokana na nafasi yake ya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB).

Soka Tanzania
Maoni