Mourinho ahukumiwa kifungo kwa kukwepa kodi

|
Jose Mourinho.

Kocha wa zamani wa Real Madrid Jose Mourinho amekuhumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kupatikana na hatia ya kukwepa kodi akiwa nchini Hispania.

Hata hivyo Mourinho hatotumikia kifungo hicho akiwa gerezani baada ya kukubali kosa kuwa alikwepa kodi katika miaka ya 2011 na 2012.

Morinho mwenye miaka 56 ametinga mahakamani leo hii mjini Madrid kuthibitishia makubaliano aliyoyafikia na mwendesha mashtaka nchini humo.

Baada ya kukubali makosa hayo Mourinho atatakiwa kulipia faini ya Euro Milioni 2 ikiwa ni sehemu ya makubaliano na mamlaka ya mapato nchini Hispania.

Soka
Maoni