Mvua yavunja yaahirisha mechi ya Simba na JKT

|
Simba walipowasili kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kuwavaa JKT Tanzania, mchezo ambao hata hivyo haukufanyika kutokana na uwanja kujaa maji.

Mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara kati ya Simba na JKT Tanzania uliokuwa uchezwe leo kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro umeahirishwa kutokana na mvua kubwa kunyesha mkoani humo.

Akizungumzia sababu za uamuzi huo, Msimamizi wa Kituo ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Soka mkoani Morogoro Charles Mwakambaya amesema kutokana na hali ya uwanja kujaa maji, wamezungumza na waamuzi, pamoja na timu zote mbili na kukubaliana kuwa mchezo huo upangiwe tarehe nyingine.

Mwakambaya amesema licha ya kanuni kuelekeza kuwa mchezo huo uchezwe siku inayofuata, hilo limeshindikana kutokana na Simba kukabiliwa na mchezo wa Kimataifa dhidi ya TP Mazembe Aprili 6 mwaka huu ambao unawahitaji kuwa si chini ya saa 72 kabla ya kuucheza.

Kuhusu mashabiki waliokuwa wameshalipa viingilio kwaajili ya mchzo huo, Mwakambaya amesema chama cha soka mkoani humo kitaweka utaratibu wa kukata kiu yao.

TPL
Maoni