Naibu waziri aridhishwa na maboresho ya Uwanja wa Nyamagana

|
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akikagua uwanja wa Nyamagana
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza jana, Jumatatu amekagua nyasi za Uwanja wa Nyamagana alipotembelea na kujionea maboresho ya uwanja huo uliogharamiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Mfuko maalumu kutoka FIFA na Halmashauri ya Nyamagana jijini Mwanza.
 
Ukarabati huo uliofanyika katika eneo la kuchezea ( Pitch) kwa kuweka nyasi bandia uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni moja.
 
Mara baada ya kukagua Naibu waziri huyo amesema, ameridhishwa na uboreshaji wa uwanja huo na kuwasihi wahusika kuutunza.
Soka Tanzania
Maoni