NBA: LeBron James Lakers kuizamisha Dallas

|
Lakers vs Dallas: LeBron James James (kushoto0 alikuwa mwiba mchungu kwa Dallas akifunga pointi 28.

Nyota wa Ligi ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani NBA, King LeBron James, amefunga alama 28 akiiongoza timu yake ya Los Angeles Lakers kushinda alama 144 kwa 103 dhidi ya wageni wao Dallas Mavericks.

Katika mchezo huo maridhawa uliopigwa usiku wa kuamkia leo, Naye Branond Ingram ameifungia Lakers alama 19.

Katika mchezo mwingine, Joel Embiid amepiga alama 16, Ben Simmons alama 13 na assists 10 wakiisaidia timu yao ya Philadelphia 76ers' kushinda alama 123 kwa 98 mbele ya Washington Wizards.

Bradley Beal angalau alikuwa na mchezo mzuri akiifungia alama 19 Wizards, licha ya kushindwa kuinusuru timu yake na kupigo cha pili mfululizo.

Hata hivyo, Washington kwa mara nyingine imecheza bila Dwight Howard ambaye anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa miezi miwili au mitatu kutokana na majeraha na pia walimkosa mchezaji wao Otto Porter Jr ambaye alikuwa na matatizo binafsi.

NBA
Maoni