Ndanda yapangua benchi lake la ufundi

|
Ndanda FC wakiwa mazoezini, Nangwanda Sijaona, Mtwara

Bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Ndanda FC yenye maskani yake mkoani Mtwara imefanya mabadiliko madogo katika benchi lao la ufundi kwa kumuweka pembeni kocha msaidizi wa timu hiyo, Hamim Mawazo.

Katibu mkuu wa Ndanda FC, Kunyangana Njowoka  ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo, amesema uongozi umefanya mabadiliko hayo kwa lengo la kuboresha na kutafuta mafanikio ya timu msimu huu.

Njowoka pia ameonesha kukerwa na kitendo cha baadhi ya wachezaji wa Ndanda kukosa nidhamu ambapo amesema uongozi hautasita kuwachukulia hatua.

Mabadiliko ya benchi la ufundi ndani ya Ndanda FC yanatajwa kuwa yataleta matokeo chanya huku uongozi wa timu hiyo ukiamini kuwa bado wana nafasi ya kufanya vizuri kwenye ligi msimu huu.

VPL
Maoni