PSG yatangaza ubingwa wa League 1 'kibabe'

|
Huu ni ubingwa wa tano kwa PSG katika misimu sita iliyopita.

Hatimaye PSG wametwaa rasmi ubingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa, (League 1) msimu wa 2017/18 kwa kishindo baada ya kuishushia Monaco kipigo cha paka cha mabao 7-1.

Mchezo huo uliokuwa mbashara ndani ya king’amuzi cha Azam TV kupitia channel ya Fox Sports, ulipigwa usiku wa jana katika dimba lake la nyumbani la Parc des Princes mjini Paris.

Mabao ya PSG yalifungwa na Giovani Lo Celso na Angel Di Maria ambao kila mmoja alifunga mawili, huku mengine yakifungwa na Edinson Cavani, Radamel Falcao aliyejifunga na Julian Draxler, wakati bao la Monaco likifungwa na Rony Lopes.

Ushindi huo umeifanya PSG ifikishe pointi 87, pointi ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote wakati zikiwa zimebaki mechi tano kwa ligi kumalizika. Timu inayofuatia ni Monaco yenye pointi 70 na Lyon iko nafasi ya tatu ikiwa na pointi 66 sawa na Marselle iliyo nafasi ya nne.

League 1
Maoni