Simba yatua Dar, sasa kukutana na Nkana ya Zambia

|
Kikosi cha Simba kilipokuwa kikianza safari kutoka nchini eSwatin

Mabingwa wa Kandanda Tanzania Bara Simba SC watakabiliana na Nkana Red Devils ya Zambia kwenye mechi mbili za raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Hatua hiyo ni baada ya mashetani hao wekundu wa Zambia kuitupa nje UD Songo ya Msumbiji kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1.

Katika mechi ya kwanza nchini Msumbuji, Nkana walishinda mabao 2-1 na katika mchezo wa maruadiano uliopigwa nyumbani kwao mjini Kitwe, Zambia, wameibuka na ushindi wa bao 1-0.

Kwa matokeo hayo, Simba na Nkana zitachuana kuwania tiketi ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ambapo mchezo wa kwanza utapigwa nchini Zambia kati ya Desemba 14 na 16, mwaka huu huku mechi ya marudiano ikipigwa kati ya Disemba 21 na 23 nchini Tanzania.

Wakati huohuo Kikosi cha Simba kimewasili leo mchana jijini Dar es Salaam kikitokea nchini eSwatin kilipoichapa Mbabane Swallows mabao 4-0 na kufuzu raundi ya kwanza kwa jumla ya mabao 8-1.

CAF
Maoni