Steven Mguto achaguliwa kuwa Mwenyekiti Bodi ya Ligi

|
Mwenyekiti wa Coastal Union Steven Mguto ambaye leo amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi.

Mwenyekiti wa Coastal Union ya Tanga inayoshiriki #LigiKuuTanzaniaBara, Steven Mguto amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB) katika uchaguzi uliofanyika leo Desemba 1, 2018 Jijini Tanga.

Awali nafasi hiyo ilikuwa ikishikiwa na aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga kabla ya TFF kumuondoa kwenye nafasi hiyo ikidai kutambua uhalali wa Yusuf Manji kama Mwenyekiti wa Yanga.  

Baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo, Rais wa Shirikisho la soka Tanzania TFF, Wallace Karia, kwenye hotuba yake amesema hatakuwa na msamaha kwa mtu yeyote atakayefanya udhadhirifu wa fedha za Shirikisho au bodi ya Ligi.

TPL
Maoni