Tanzania yapata dhahabu, riadha ya majeshi EAC

|
Kocha Mkuu wa Mchezo wa Riadha kwa Jeshi la Polisi Tanzania, Rogart Stephen.

Michezo ya Majeshi ya Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati imeingia katika siku ya tatu hii leo huku Tanzania ikipata medali ya dhahabu katika mbio za mita 5000.

Akizungumza na Azam Sports leo, kocha mkuu wa mchezo wa riadha kwa Jeshi la Polisi Tanzania, Rogart Stephen, amesema baada ya kufanya vizuri katika mbio fupi zilizofanyika kwenye uwanja wa taifa ana matumaini makubwa ya Tanzania kutang’ara katika mbio ndefu za cross country zitakazofanyika Ijumaa hii katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani.

Amesema licha ya mbio hizo kutawaliwa na Wakenya, timu yake imejipanga kuwaonesha kuwa Tanzania pia ina uwezo kwenye mchezo wa riadha.

Michezo hiyo ya Majeshi ya Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki inaendelea Ijumaa hii kwa timu za polisi za nchi hizo kupambana katika michezo mbalimbali.

Michezo
Maoni