The Emirates FA Cup: Tottenham Hotspur yatinga mzunguko wa nne kibabe

|
Ushindi wa 7-0 ndio ushindi mkubwa zaidi kwa Tottenham Hostspur tangua kuanzishwa kwake mwaka 1882.

Mshambuliaji wa Hispania, Fernando Llorente ameongoza mauaji kwa klabu ta League Two ya Tranmere Rovers akifunga hat-trick na kuisaidia Tottenham Hotspur kutinga mzunguko wan ne wa kombe la FA.

Llorente, aliyeanza kwa mara ya pili kwenye kikosi cha Spurs katika msimu huu, alifunga mabao hayo ndani ya dakika 24 kwenye ushindi wa kihistoria tangu kuanzishwa kwake.

Katika dakika ya 48, Llorente alifungua ukurasa wake wa mabao akimalizia kazi ya mshambualiaji Son Heung-min kabla ya kuiga mpira wa chini chini uliompita kipa wa Tranmere Scott Davies akimaliza pasi ya Oliver Skipp.

Dakika moja baadae, Mhispania huyo alihitimisha kalamu yake ya mabao “aki-sukuma ndani” krosi ya Lucas Moura kabla ya kumpisha nahodha wa England Harry Kane ambaye pia alifunga bao la saba lililoifurumisha nje ya mashindano Tranmere.

Mlinzi wa pembeni wa Spurs kutoka nchini Ivory Coast, Serge Aurier alifungua kalamu ya mabao kwenye dakika ya 40 kwa shuti la umbali wa yadi 25 lililompalaza mlinzi wa Tranmere, Emmanuel Monthe na kumpoteza golikipa wa timu hiyo na kumuacha akishindwa kufanya lolote.

Goli la kwanza la Llorente lilikuwa la kwanza katika mabao matatu ndani ya dakika tisa likifuatiwa na mabao ya Aurier aliyepachika bao lake la pili kabla ya Son kufunga bao la juhudi binafsi.

Nahodha wa England, Kane alifunga bao la kukamilisha kalamu kwenye dakika ya 82 akifikia rekodi ya ufungaji mabao kwa timu ya Spurs sawa na Cliff Jones wote wakiwa na mabao 159.

Leo ni zamu ya miamba wengine wa Englan, Manchester United, Chelsea na Arsenal watakaotupa karata zao kuanzia saa 9:30 Alasiri kwa saa za Afrika Mashariki na mechi zote hizo zitakuwa MBASHARA ‘LIVE’ ndani ya chaneli ya AzamSports2.Totte

Soka
Maoni