Vilabu 29 kuwania ubingwa wa Afrika Kanda ya Tano, Dar es Salaam

|
Phares Magesa, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF)

Zaidi ya klabu bingwa 29 za mchezo wa mpira wa kikapu kutoka nchi wanachama wa kanda ya tano ya Afrika zimethibitisha kushiriki michuano ya klabu bingwa ya Afrika kanda ya tano itakayofanyika nchini kuanzia Septemba 30 mwaka huu.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Pharess Magesa, amasema maandalizi ya michuano hiyo itakayofanyika uwanja wa ndani wa taifa jijini Dar es Salaam yamekamilika.

Magesa pia amewaomba wadau kuchangia kwa hali na mali ili mafanikio yapatikane na malengo yaliyokusudiwa yafikiwe.

Kikapu
Maoni