Warriors yaanza kwa kishindo fainali ya kihistoria NBA

|
Mchezo wa Kikapu nchini Marekani

Golden State Warriors imeanza vyema kampeni yake ya kulisaka taji la ubingwa wa Mpira wa Kikapu Nchini Marekani (NBA) msimu huu kwa kuwabamiza wapinzani wao Cleveland Cavaliers kwa vikapu 113 kwa 91.

Ushindi huo ni katika mchezo wa kwanza wa fainali kati ya jumla ya michezo 7 inayotarajiwa kupigwa, ambapo Kevin Durant ameibuka kinara kwa kufunga jumla ya vikapu 38, rebound 8 na assist 8 wakati nyota mwingine Stephen Curry akifunga vikapu 28, na assist 10..

Mchezo huo uliochezwa alfajiri ya leo, Ijumaa umeandika historia katika Ligi ya Kikapu nchini humo kwa timu mbili kukutana katika fainali kwa misimu mitatu mfululizo.

Mwaka 2015, timu hizo zilikutana na kushuhudiwa Golden State wakiibuka mabingwa huku mwaka 2016 Cavaliers wakilipiza kisasi. Kwa mwaka huu bado michezo 6 kuamua ni nani ataibuka mshindi mpya wa ligi hiyo.

Kikapu
Maoni