Test
Cirque du Soleil kuonesha maigizo ya maisha ya Lionel Messi

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina na nyota wa mabingwa wa Hispania, Barcelona Lionel Messi anatarajia kuigizwa kwenye onyesho la vikaragosi la Cirque du Soleil.

Kundi hilo linatarajia kuwa na onyesho la kimataifa mwakani na limeahidi kufanya “tafsiri ya kisanii ya maisha na kipaji cha hali ya juu cha Lionel Messi”

Cirque du Soleil lenye makazi yake nchini Marekani kwenye mji wa Montreal limewahi kuwaigiza mastaa wengine wengi wakiwemo wa kundi la muziki wa rock la Uingereza la The Beatles na mfalme wa Pop duniani, Michel Jackson.

Lionel Messi akizungumzia onesho hilo amesema "Inachanganya, ni kama jambo la pekee sana lakini ni kama wendawazimu kuona Cirque du Soleil watatengeneza onesho kwa kuangazia maisha yangu, ninachokipenda na mchezo wangu,”.

Messi mwenye tuzo tano za dunia za Ballon d'Or ameelezea maonesho ya kundi hilo kama “kipindi pendwa” nyumbani kwake.

"Sina mashaka onesho hilo litawaacha watu midomo wazi kama ambavyo maonesho yao mara zote hufanya hivyo." Aliongeza Messi

Eden Hazard akiri kuchanganyikiwa juu ya kubaki Chelsea au kujiunga Madrid

Kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji Eden Hazard amesema ‘anachanwa chanwa’ na uamuzi anaopaswa kuchukua kati ya kuongeza mkataba na klabu yake ya sasa ya Chelsea au kujiunga na Real Madrid.

Hazard anatarajiwa kuingia kwenye mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Chelsea mwishoni mwa msimu huu lakini ameendelea kusisitiza asingependa kupita njia aliyoichagua aliyekuwa shujaa wa miamba hiyo ya London, golikipa Thibaus Courtois aliyelazimisha auzwe kwa miamba ya Hispania Real Madrid.

Kiungo huyo aliyeisaidia Ubelgiji kushika nafasi ya tatu kwenye Kombe la Dunia, amesisitiza kuwa yuko tayari kujadiliana juu ya mkataba mpya na Chelsea.

Tetesi za staa huyo aliyeanza msimu huu vizuri akiwa na magoli manane katika mechi 10 alizoheza msimu huu za kuhamia Hispania zilianza kusambaa mwishoni mwa msimu uliopita na wakati wa Kombe la Dunia alithibitisha kutamani kujiunga na Real Madrid.

"Ndio maana nilisema baada ya Kombe la Dunia na nilisema, nafikiri ni wakati wa kubadilisha mazingira kwasababu nilikuwa na wakati mzuri kwenye Kombe la Dunia” alisema Hazard

"Niko vizuri sana kimchezo kwa sasa, ninacheza soka maridadi sana. Real Madrid ni klabu bora zaidi duniani. Sitaki kudanganya hii leo.

"Ni ndoto yangu tangu nikiwa mtoto. Nilikuwa naiota klabu hii. Sitaki kuzungumzia hilo kila siku. Tutaona kitakachotokea” Aliongezea

Hazard ameshinda mataji mawili ya Ligi Kuu Uingereza ‘Premier League’ akiwa na Chelsea, kombe la FA, kombe la Ligi na kombe la Europa.

Modric amfunika Ronaldo kwa mara nyingine

Kiungo wa kimataifa wa Croatia Luka Modric amewashinda Cristiano Ronaldo na Mohamed Salah na kushinda tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa FIFA.

Modric ameshinda tuzo hiyo kufuatia kuwa na msimu wenye mafanikio makubwa akiwa na Real Madrid kwa kuisaidia miamba hiyo ya Hispania kutwaa ubngwa wa tatu mfululizo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL).

Mchango wake pia katika kombe la dunia umepongezwa kwa kuiongoza timu ya Croatia kucheza fainali ya kombe hilo kwa mara ya kwanza na licha ya kufungwa na Ufaransa lakini Modric alitwaa tuzo ya Golden Ball.

Hata hivyo sherehe hizo ziliingia doa baada ya Ronaldo aliyekuwa akitajwa sana kustahili tuzo hiyo kwa kushinda taji la tano la UCL kutooneka kwenye ukumbi wakati wa utoaji wa tuzo hizo kutokana na kubanwa na ratiba za katikati ya wiki zinazoikabili timu yake ya Juventus.

Baada ya kupokea tuzo hiyo, Modric alitoa heshima kwa aliyekuwa nahodha wa taifa hilo kwenye fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1998, Zvonimir Boban, aliyemtaja kuwa shujaa wake.

"Ndiye aliyenihamaisha sana na kikosi chao ndicho kilichotupa Imani kuwa tunaweza kufanikiwa kushinda kitu kikubwa nchini Urusi. Ni matumaini yangu tutakuwa hivyo kwa vizazi vijavyo” alisema Modric.

"Tuzo hii inadhihirisha sote tunaweza kuwa chochote tutakacho tukifanya juhudi, tukijitoa na tukiamini. Ndoto zote hutimia”

Mshambuliaji wa Misri, Mohamed Salah alifanikiwa kutwaa tuzo ya goli bora zaidi kutokana na goli aliloifungia timu yake ya Liverpool dhidi ya wapinzani wao wa jadi Everton.

Kipa wa zamani wa Chelsea aliyehamia Real Madrid, Thibaut Courtois alishinda tuzo ya golikipa bora kutokana na kiwango alichokionyesha wakati wa kombe la dunia huku tuzo ya kocha bora ikitwaliwa na Didier Deschamps wa Ufaransa aliyeliongoza taifa hilo kutwaa ubingwa kwa kuifunga Croatia.

Brazil ndiyo timu yenye mafanikio zaidi - Kocha Tite amjibu Trump

Kocha wa Mkuu wa timu ya Taifa ya Brazil, Adenor Leonardo Bacchi maarufu kama Tite, amemjibu Rais wa Marekani Donald Trump kuwa Brazil ndiyo timu yenye mafanikio zaidi duniani kwa kutwaa kombe la dunia mara tano.

Majibu hayo ya Tite yamekuja siku chache baada Donald Trump kuidhihaki Brazil kuwa ina matatizo kiasi cha kutolewa kwenye robo fainali ya kombe la dunia na timu ya Ubegiji.

Trump alitoa kauli hiyo wakati akimpokea Rais FIFA Giann Infatino alipozulu Marekeni kutambulisha kombe la dunia litakalofanyika Marekani mwaka 2026.

Kauli hiyo imeonekana kumkera kocha Tite ambaye leo kwenye mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mechi ya kirafiki dhidi ya El Salvador, ameonesha ishara ya vidole vitano ikiwa ni jibu kwa Trump kuwa Brazil ndiyo timu yenye mafanikio zaidi duniani ikiwa imetwaa mara nao kombe la dunia.

Maradona kocha mpya wa Dorados ya Mexico

Klabu ya soka ya Dorados ya nchini Mexico imemuajiri Diego Armando Maradona kuwa kocha Mkuu wa klabu hiyo.

Maradona aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Culiacan na kupokewa na kundi kubwa la mashabiki wa timu hiyo.

Mashabiki wa Dorados wameonekana kufurahishwa na ujio wa Maradona wakiwa wameshika vitambaa vyenye ujumbe usemao Daima tuko na wewe.

Mashabiki wengine walishika picha ya Maradona yenye maneno kama "Bosi amewasilia" na "Diego yuko nyumbani".

Kitendo cha Maradona kurudi Mexico kimeibua msisimko na kumbukumbu ya mwaka 1986 pale jemedari huyo alipoiongoza Argentina kutwaa kombe la dunia katika fainali zilizofanyika nchini humo akifunga goli maarufu la ‘Mkono Mungu’.

Changamoto pekee inayotazamiwa kumkumba Maradona ni kuwa anatajwa kuwa mtumiaji wa dawa za kulevya na timu anayokwenda kufundisha ya Dorados ipo katika mji wa Sinaloa mji ambao unaogoza kwa uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya

Kocha wa Real Madrid, Julen Lopetegui "Sijutii kutimuliwa Hispania"

Kocha wa Real Madrid Julen Lopetegui amesema hajutii kufukuzwa kuifundisha timu ya taifa ya Hispania siku chache kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia.

Shirikisho la soka la Hispania, lilimfuta kazi Lopetegui baada ya kukiri kuingia mkataba kwa (kwa siri) wa kuchukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa miamba hiyo, Zinedine Zidane.

"Nilichofanya ni kuchukua uamuzi na nitachukua uamuzi kama huo mara nyingine, nilifanya hivyo kwa namna ya uaminifu wa juu kabisa na sijutii chochote” aliiambia redio Onda Cero ya Hispania.

"Nina furaha kubwa kuwa kocha wa Real Madrid, tunachangamoto maalum na malengo makubwa. Kilichotokea kimetokea na hakiwezi kubadilishwa”

Hispania iliyokuwa miongoni mwa timu zilizotarajiwa kushinda kombe la dunia lakini iliangukia pua mbele ya wenyeji Urusi kwa mikwaju ya penati kwenye hatua ya 16-bora.

Siku ya kutambulishwa kwake katika uwanja wa Santiago Bernabeu, siku moja baada ya kutimuliwa kuifundisha Hispania, Lopetegui alisema, "jana ilikuwa siku mbaya zaidi kwenye maisha yangu, leo ni siku bora zaidi”

Hispania imeanza zama mpya na aliyekuwa mshambuliaji wa Barcelona na timu ya Hispania, Luis Enrique aliyekabidhiwa timu hiyo baada ya kombe la dunia.

Allegri amuonya Ronaldo "Serie A, si ya kufunga mabao 40"

Kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri ameweka wazi kuwa ni vigumu kwa mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Cristiano Ronlado kufunga magoli 40 katika ligi ya Italia maarufu kama Serie A.

Hadi sasa Ronaldo hajafanikiwa kufunga goli hata moja katika mechi tatu ambazo Juventus wamecheza.

Licha ya kutofunga goli, Allegri alimsifu Ronaldo kwa kuonesha kiwango kizuri katika mchezo dhidi ya Parma siku ya Jumamosi.

“Alicheza vizuri, lakini hapa Italia timu nyingi zimejizatiti zaidi kwenye mchezo wa kujilinda nadhani hata yeye (Ronaldo) analifahamu hilo, ni mchezaji mwerevu.

“Italia ni vigumu kufunga magoli 40 (kwa msimu mmoja).” Alisema Allegri baada ya timu yake kuibuka na usindi wa 2-1 dhidi ya Parma.

Ronaldo alihamia Juventus akitokea Real Madrid ya Hispania kwa kilichodaiwa hofu ya kumkimbia mshambuliaji aliyetarajiwa kusajiliwa na miamba hiyo ya Hispania kati ya Neymar Jr au Mbappe.