Yanga yalazimishwa sare tena na Ndanda SC

|
Ilipotokea penati ya Yanga dakika ya 28.

Ndanda SC ‘Wanakuchere’ wameilazimisha sare ya bao 1-1 Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Ndanda ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 20 kupitia kwa Vitalisy Mayanga lakini Yanga wakasawazisha kwa kichwa cha Papy Tshishimbi aliyemalizia krosi ya Kelvin Yondan dakika ya 62.

Hata hivyo dakika ya 29 Yanga walipoteza nafasi ya bao baada ya Amissi Tambwe kukosa mkwaju wa penati waliyoipata kutokana na Heritier Makambo kuchezewa rafu ndani ya eneo la hatari. 

Matokeo haya ni sawa na yale ya raundi ya kwanza kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam ambapo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Matokeo hayo yameendelea kuiweka Yanga kileleni licha ya kupunguzwa kasi yake, sasa ikifikisha pointi 68, mbele ya Azam FC wenye pointi 62 huku Ndanda SC wakifikisha pointi 37 na kusogea hadi nafasi ya 11 kutoka nafasi ya 15.

TPL
Maoni