Yanga yazidi kuonesha ukomavu ligi kuu, yaipiga KMC 2-1

|
Kipa wa KMC Juma Kaseja baada ya bao la pili ambalo lilikuwa ni la kujifunga kupitia kwa beki wake Ally Ally.

Mabingwa wa Kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC wameendelea kuwa mwiba kwenye ligi hiyo msimu huu baada ya leo kuigaragaza KMC kwa kipigo cha mabao 2-1, mchezo ukipigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

KMC ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 17 kupitia kwa Mohamed Rashid, kabl aya Yanga kusawazisha dakika ya 37 kupitia kwa Papy Tshishimbi.

Dakika ya 67 beki wa KMC Ally Ally akaipa Yanga bao la pili kwa kujifunga, mpira uliopigwa na Ibrahim Ajibu. 

Katika mchezo mwingine Mwadui FC imepata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, mkoani Shinyanga.

Mbeya City ndiyo waliotangulia kupata bao kupitia kwa Frank Ikobela dakika ya 19, kabla ya Mwadui  kusawazisha dakika ya 22 kupitia kwa Revocatus Richard na kuongeza mengine kupitia kwa Salim Aiyee dakika ya 84 na Wallace Kiango dakika 90+2.

TPL
Maoni